ZILIZOFANYA VYEMA WIKI HII

Bingwa - - SPORTS -

SOZA MFUHA

Kisa cha filamu hii kinazungumzia mtu (Soza) aliyedhaniwa kwamba amefariki dunia, lakini bado anasumbua watu kwa kuonekana mitaa mbalimbali ya Bagamoyo akiwa hai na kuwapa mashaka wanakijiji na kujikuta wakiishi kwa hofu.

MANENTO

Filamu hii yenye kisa cha kisasi cha mapenzi ambayo yameleta purukushani baina ya vijana wawili ambao walikuwa wakimgombania msichana mrembo imetoka wiki iliyopita na kuanza kufanya vizuri sokoni. Imechezwa na wasanii Patcho Mwamba, Frasisco Mwinuka ‘Piere’, Penina na wengine wengi.

SOZI

Ni filamu yenye kisa cha ndoto za kichawi zinazogeuka kuwa ukweli na kuathiri maisha halisi. Filamu hii imechezwa kwa kufuata maadili ya Kitanzania na inaweza kuangaliwa na familia. Wasanii walioigiza kwenye filamu hiyo ni Hisani Muya ‘Tino’ na wengineo.

KACHU MSELA

Hii ni filamu ya vichekesho ambayo imefanya vizuri sokoni kwenye mauzo na kutazamwa sana kwenye vibandaumiza na sehemu nyingine zinaonyeshwa filamu ikiwamo majumbani. Filamu hii imechezwa na Tin White na Ringo wakimshirikisha Tausi Ally.

WHY

Hii ni filamu ya kwanza ya Bongo Movie kuchezwa kwenye ndege. Kisa cha filamu hii kinahusiana na ndoa ambayo inaingia kwenye utata kutokana na mwanamke kumnyanyasa mumewe. Filamu hii imchezwa na wasanii kama Shamsa Ford, Hisani Muya ‘Tino’, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na itasambazwa na Florian Flowerence.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.