MAISHA MAGUMU ILA BATA ZINALIKA

Bingwa - - IJUMAA SPESHO HAPA BATA TU - NA KYALAA SEHEYE

INGAWA hali ngumu lakini bata zinasongeshwa kama kawaida kwenye pande mbalimbali.

Watu wanajiachia na kula bata mpaka unashangaa fedha wametoa wapi, lakini ndio mambo ya mjini kila mtu na mipango yake ya kusaka noti, cha msingi usikate tamaa na wewe uzikamate.

Hivyo bila kujali umefulia au unazo, kama kawaida Hapa Bata Tu tunakupa ratiba za maeneo mbalimbali ya kula bata na kupoza msongo wa mawazo unaotokana na ugumu wa maisha na uchovu wa kusaka ‘money’.

MUSOMA NA KAHAMA

Baada ya tamasha la muziki la Fiesta Tumekosoma kuzinduliwa wiki iliyopita mjini Arusha, leo litawasha moto Musoma katika Uwanja wa Kambarage.

Nao wakazi wa Kahama watafurahia tamasha hilo litakalofanyika Jumapili katika Uwanja wa Taifa wa Kahama.

Wasanii kama Chege, Shilole, Nandy, Roma na Stamina ‘Rostam’, Young Dee na wengine wengi watatoa burudani.

MAISHA BASMENTMAKUMBUSHO

Jumamosi hii itakuwa zamu ya Snura Mushi kutoa burudani, ambapo atazindua wimbo wake mpya uitwao Zungusha ambao amemshirikisha Christian Bella, akisindikizwa na Roma Mkatoliki ‘Mzee wa Zimbabwe’.

AFRICAN STARS –TWANGA PEPETA

Baada ya ‘show’ zao za kila Alhamisi katika Ukumbi wa Monie Juction maeneo ya Jet Lumo, Ijumaa hii watakuwa Bulyaga, Temeke na Jumamosi wataendelea kuuaga Ukumbi wa Mango Garden, ambao unatarajiwa kuvunjwa na kujengwa majengo mengine ya kibiashara.

Wikiendi wataimalizia kwenye Ukumbi wa Brazil Pub uliopo Tegeta Kibo.

DAR LIVE-MBAGALA

Jumamosi hii katika ukumbi huo kutakuwa na onyesho la Usiku wa Kukumbuka za Zamani, ambapo Jahazi Modern Taarab wataangusha bonge la burudani wakiongozwa na Abubakary Soud ‘Amigo’, huku kukiwa na waimbaji waalikwa kama Mohamed Ally ‘Mtoto Pori’, Fatma Mcharuko, Khadija Yusuph, Rahma Machupa na Miriam Amour.

GARDEN BREEZ- MAGOMENI HOSPITALI

Bendi ya Mapacha Watatu inafanya bonanza kila Jumapili katika viwanja vya Garden Breez vilivyopo katika Hospitali ya Magomeni, ambapo kutakuwa na michezo ya watoto na usiku ndio burudani kwa wakubwa.

WAKALI WAO MODERN TAARAB

Kila Jumanne wanapatikana Manzese Friends Corner kwenye Baa mpya na wanakuwa na mashindano ya mkali wa Singeli na kutakuwa na washiriki 12.

MLIMANI CITY- CENTURY CINEMA

Leo Ijumaa ‘movie’ ya Brigsby Bear itaonyeshwa na filamu nyingine kali.

RIVER ROAD- KIBAHA PICHA YA NDEGE

Leo Ijumaa kutakuwa na shindano la muziki wa Singeli, ambapo mshindi atapata nafasi ya fedha na kurekodi nyimbo mbili, mshindi wa pili atarekodi wimbo mmoja na wa tatu fedha.

Kesho kutashushwa disko bab kubwa na Madj wakali na wanawake wa mwanzo 20 wataingia bure.

BONAG HOTEL- KILUVIA GOGONI

Leo kutakuwa na disko bab kubwa litakaloshushwa na Madj wakali na kesho itakuwa ni muziki wa ‘live’ utakaoshushwa na bendi ya hoteli hiyo.

ivyo bila kujali umefulia au unazo, kama kawaida Hapa Bata Tu tunakupa ratiba za maeneo mbalimbali ya kula bata na kupoza msongo wa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.