Pungwa ni ngoma ya kukabidhiana uganga

Bingwa - - IJUMAA SPESHO HAPA BATA TU - NA KYALAA SEHEYE

LEO safu ya Ngoma Zetu imetinga hadi Tanga na kusimuliwa ngoma ya Pungwa ambayo hutumiwa sana na makabila ya Wasambaa, Wabondei na Wazigua kidogo.

Ngoma hii ni kwa wale watu wanaoamini mambo ya kishirikina na inapopigwa ujue kuna mtu anakabidhiwa mikoba ya uganga au kifaa chochote kama pete nakadhalika.

Pia hupigiwa mtu ambaye anaumwa sana na ameenda kwa mganga na kupandisha mashetani na kuagiza apewe kitu aidha pete au mfuko wa uganga.

Pungwa haina kipindi maalumu wala muda wa kupigwa, ila hupigwa na wanaume na mara nyingi wanaokuwa wanapigiwa ngoma hizo ni wanawake.

Hakuna mfumo wa kucheza ngoma hii, ila watu mbalimbali wanajumuika na inapopigwa mhusika anayepigiwa atapandisha mashetani na kuongea mambo mbalimbali, lakini wale wageni na ndugu waliohudhuria wanaweza kupandisha mashetani na wao.

Kunakuwa na vyakula mbalimbali wakati wa ngoma hiyo ambayo inakuwa kama sherehe kwa wenyewe wenye imani na mambo hayo ya uganga na ushirikina.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.