Hali ya Mc Pilipili yazidi kuimarika

Bingwa - - IJUMAA SPESHO PAPASO LA BURUDANI -

NA CHRISTOPHER MSEKENA

BAADA ya kupata ajali ya gari katikati ya kijiji cha Nyasamba na Bubiki, mkoani Shinyanga na kukimbizwa Hospitali ya Bugando, Mwanza kwa matibabu, mchekeshaji na mshereheshaji ghali nchini, Emmanuel Mathias ‘Mc Pilipili’ hali yake imezidi kutengamaa.

Mpiga picha wa Mc Pilipili, Lumato, ameliambia Papaso la Burudani kuwa, bosi wake anaendelea kupata matibabu na afya yake inazidi kuimarika, hivyo Watanzania waendelee kumwombea arudi kwenye hali yake ya kawaida.

“Anaendelea kupata matibabu, Watanzania waendelee kumwombea, aliumia japo si sana, alipatwa na mshtuko na majeraha yaliyotokana na ajali, hata dereva wake pia anaendelea vizuri, tuendelee kuwaombea kwa Mungu,” alisema Lumato.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.