BET NA MZEE WA KUBETI MARA PAAP! MHINDI KAKAZA TENA

Bingwa - - IJUMAA SPESHO -

NAAM, ni siku nyingine tena tunayokutana kwenye kipande chetu hiki cha kubeti, kusuka mikeka kuntu ili mambo yakawe sawa wikiendi hii.

Kuna waliocheka wiki hii katika zile mechi za Uefa ila kuna waliolizwa, nafahamu nini cha kufanya ili wikiendi hii mcheke kwa pesa za Mhindi. Hebu cheki na hizi dondoo nne.

Tottenham v Swansea Spurs inaonekana kuanza kuuzoea uwanja wa Wembley, kufuatia ushindi mnono dhidi ya Dortmund juzi, kazi ipo kwa Swansea, aidha wapambane wapate ushindi au sare, ama wakubali kuangamizwa na vijana hao wa Mauricio Pochettino ambao hawatataka kujitetea kwamba uwanja huo kwao ni nuksi kwa kusakata soka safi.

Tegemea Swansea itakayocheza kwa kujilinda zaidi ya Tottenham na licha ya kwamba wana kipa mzuri, Peter Fabianski, sidhani kama ataweza kuwazuia Harry Kane, Dele Alli na Christian Eriksen, wafanye yao, takwimu zinaonesha Swansea wamefungwa mechi 10 kati ya 12 walizocheza nao wakali hao wa London.

Utabiri: Spurs 4-0 Swansea Liverpool v Burnley Majogoo wa Anfield wataikaribisha Burnley kesho, je, wataweza kurudi kwenye hali yao baada ya kucheza mechi mbili za Ligi Kuu England na UEFA. Moja wakifungwa na nyingine sare (wakifungwa mabao saba na kufunga mawili), Burnley inaweza kuwa timu yenye bahati wikiendi hii.

Burnley wataingia Anfield wakiwa na mwenendo mzuri, ambapo baada ya ule ushindi wa bao 3-2 dhidi ya Chelsea ukifuatiwa na kichapo cha bao 1-0 dhidi ya West Brom, walirudi vizuri kwa kuwachapa Blackburn, sare dhidi ya Spurs na kushinda dhidi ya Crystal Palace, lakini Liverpool wana rekodi ya kushinda mechi tano kati ya sita za mwisho dhidi ya yao.

‘The Clarets’ hao siku hizi wanajitahidi sana kufunga ugenini, mabao 12 katika mechi 14 za mwisho za Premier League, clean sheets zikiwa tatu huku Liverpool ikiruhusu nyavu zao kutikiswa mara 11 katika mechi 16 za mwisho wakiwa Anfield ila ni mechi moja tu waliyoshindwa kufunga bao, kesho kuna dalili za wao kukamatwa pale ikizingatiwa uchovu wa kucheza ligi ya mabingwa na ‘double chance’ pia naiona imekaa vizuri kwa Burnley.

Utabiri: Liverpool 1-1 Burnley Chelsea v Arsenal Wapinzani wa jadi hawa wa London watazichapa mchana kweupe, baada ya kila mmoja kucheza mechi nne, katikati hapo walizua maswali kama kweli wapo tayari kuwania taji la EPL msimu huu.Ila maswali muhimu ya kujiuliza ni kama Chelsea wataweza kuendeleza kushinda kwa mabao mawili kila mechi? Arsenal watavuja tena kwenye safu yao ya ulinzi.

Mabingwa watetezi wana rekodi nzuri ya London Derby hii hasa kwenye Ligi Kuu England, wakishinda zote tano za mwisho na wataingia kwenye mchezo huo na lengo moja la kusaka pointi tatu nyumbani ila mtihani upo kwenye safu yao ya ulinzi ambayo ina upya-upya, dhidi ya Arsenal yenye mastraika watano wazima na wenye uwezo wa kucheka na nyavu. Nao pia safu yao ya ulinzi imekosa ushirikiano na mipango madhubuti hivyo kila timu ina nafasi ya kutupia bao.

Cha kuzingatia, timu yoyote itakayokuwa ya kwanza kufunga bao haitapoteza mchezo huo.

Chelsea 3-1 Arsenal

Man Utd v Everton Swali kubwa lililoniibukia kuhusu huu mchezo ni kama timu zote zitakuwa fiti asilimia 100 kufuatia mechi zao za Ulaya.

Timu zote zilikuwa kwenye majukumu katikati ya wiki hii, hivyo lazima kuna uchovu utakaoathiri matokeo keshokutwa. Ila tukianza kuzitazama facts, Man Utd imeweza kufunga bao kwenye kila mchezo msimu huu wakiwa na wastani wa bao tatu huku Romelu Lukaku akiwa on fire.

Mchezo huo una dalili chache sana za kutoa sare, mshindi atapatikana ila tuzingatie kwamba Man Utd ndiyo timu inayoongoza kwa clean sheet sambamba na Huddersfield sambamba na kufunga mabao mengi huku Everton, wakiingia Old Trafford na rekodi ya kufungwa mechi 18 kati ya 25 za mwisho.

Utabiri: Man Utd 2-0 Everton

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.