SARE YA LIVERPOOL DHIDI YA SEVILLA NI YA KUSIKITISHA

Bingwa - - HABARI -

RASMI mbio za kuwania taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya zilianza mapema wiki hii na vigogo wa soka ndio waliotikisa vyombo vya habari kwa kuibuka na ushindi mnono katika michezo yao hiyo ya ufunguzi.

Aidha, nyota wenye majina makubwa nao walifanya yao. Msimu huu mbona tutatafutana!?

Baada ya wiki hii kushuhudia burudani za kufungulia msimu wa ligi ya mabingwa, kwa sasa tunasubiri hadi wiki mbili zipite ndio tuje kuwaona tena akina Harry Kane wakitikisa nyavu kama vichaa!

Ligi Kuu England nayo ilikuwa na cha kujisifia katika mechi za michuano hiyo, baada ya wawakilishi wao wanne kati ya watano kuibuka na ushindi mnono katika mechi hizo.

Klabu za Man United, Chelsea, Man City na Tottenham zilishinda mechi zao za awali, huku mabingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita, Chelsea, wakitia fora kwa kuwanyuka wageni wa michuano, Qarabag kwa mabao 6-0.

Lakini hadithi ilikuwa tofauti kwa wawakilishi wengine wa ligi hiyo, Liverpool, ambao walilazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Sevilla katika mtanange uliopigwa kwenye dimba la Anfield.

Majogoo hao waliokuwa wakitabiriwa kuonesha kiwango kizuri msimu huu ikizingatiwa ni muda mrefu tangu washiriki mara ya mwisho, lakini waliendelea kuonesha mapungufu yale yale na kuzua maswali kama kweli watafika kokote?

Kikosi hicho kilionekana kucheza soka safi na kuwamiliki wapinzani wao hao, lakini kadiri dakika zilivyokuwa zikisonga, vijana hao wa kocha Jurgen Klopp, walisinzia na kupoteza uongozi

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.