ANTHONY JOSHUA AMLILIA KLITSCHKO

Bingwa - - HABARI/MAKALA -

LICHA ya pambano lao kuota mbawa, bondia Anthony Joshua amesema angetamani kuzichapa kwa mara ya pili na mkongwe huyo.

Joshua alimchakaza

Klitschko katika pambano la kwanza na kulikuwa na madai kwamba wangerudiana Novemba 11, mwaka huu, lakini wakati wengi wakisubiri, mpinzani wake huyo alitangaza kutundika daluga.

Nyota huyo, Joshua, anajiandaa kuzitwanga na Kubrat Pulev, pambano litakalofanyika mjini Cardiff, Oktoba 28.

Ingawa wengi wanaliona pambano hilo kuwa ni jepesi, ukweli ni kwamba Pulev amepoteza pambano moja pekee tangu alipoanza kupanda ulingoni na lilikuwa ni dhidi ya Klitschko mwaka 2014.

Katika pambano hilo, litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Principality, Joshua atakuwa anasaka ushindi wake wa 20 kwa ‘KO’.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.