Roma, Nandy, Fid Q, Saida Karoli kukinukisha Fiesta Musoma leo

Bingwa - - HABARI/MAKALA -

TAMASHA la muziki la Tigo Fiesta, leo linatarajiwa kuhamia mjini Musoma katika Uwanja wa Karume, ikiwa ni baada ya kukonga nyoyo za wakazi wa Arusha mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Katika tamasha lililofanyika Arusha ambalo ni la uzinduzi wa msimu huu, msanii wa Bongo Fleva, Ali Kiba, alifunika vilivyo na wimbo wake wa Seduce Me ambao kwa sasa ndio habari ya mjini kutokana na kuwagusa wengi.

Mbali ya Ali Kiba, wasanii wengine waliopagawisha ni Roma Mkatoliki, Joh Makini na kundi lake la Weusi, Ben Pol na wengineo kibao waliopanda jukwaani siku hiyo.

Na sasa tamasha hilo linahamia Musoma, mji huo ukiwa ni sehemu ya miji mingine 14 iliyopabngiwa kupata uhondo wa tamasha hilo kubwa kabisa la burudani la kila mwaka ambalo msimu huu, limepata udhamini mnono wa kampuni ya simu za mikononi ya Tigo Tanzania.

Akizungumzia tamasha hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Fiesta, Sebastian Maganga, alisema kuwa wakazi wa Musoma watarajie burudani ya aina yaek leo kutoka kwa wasanii wao wakali wa hapa nchini.

Anasema kuwa Tigo Fiesta ni burudani ya kipekee ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki na kwamba mashabiki wa Arusha wamefurahia mno burudani waliyoipata ambayo itaendelea katika mikoa mingine.

“Tutawaletea wasanii wenye hadhi kulingana na mapendekezo ya mashabiki husika wa mkoa huo, tena wale waliojizolea sifa ndani na nje ya nchi,” anasema Maganga.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugrenzi wa Masoko wa Tigo, William Mpinga, anasema kuwa tamasha la Tigo Fiesta lina kaulimbiu ya ‘Tumekusomaa’, msemo huo ukilenga kuwainua vijana wote wanaofanya muziki lakini hawajapata nafasi ya kuonekana au kupata ufadhili, hii ikimaanisha kwamba watakuwa wanawasoma hao vijana kutoka maeneo waliyopo. Anasema kuwa tamasha hilo litakavyoambatana na misisimko kibao katika mikoa 15 litakakopita, litakuwa tamasha kubwa na la kusisimua zaidi katika historia ya miaka 16 ya tamasha hilo la kitamaduni katika ukanda huu wa Afrika.

Aliwataja wasanii watakaopanda jukwaani leo kuwa ni Roma Mkatoliki, Rostam, Darassa, Stamina, Shilole, Nandy, Ben Pol, Jux, Saida Karoli, Joh Makini, Fid Q, Stamina, Mr Blue, Ditto, Dulla Makabila na wengineo.

Mpinga alisema kuwa baada ya wasanii hao kuuwasha moto Musoma, Jumapili watahamia Kahama na burudani hiyo kuendelea katika mikoa ya Mwanza, Tabora na Dodoma.

Maeneo mengine ni Iringa, Songea, Njombe, Sumbawanga, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Mtwara na kuhitimishwa jijini Dar es Salaam.

“Kwa mara ya kwanza kabisa tutafanya tamasha letu hili pale mkoani Njombe, hii yote ni katika kuhakikisha kwamba tunawapatia washabiki wetu burudani ya uhakika katika maeneo mengi zaidi,” anasema.

“Kupitia Tigo Fiesta 2017Tumekusoma, Tigo imejikita kuinua vipaji vya wasanii wa Kitanzania kama njia mojawapo ya kukuza sanaa nchini. Kama tunavyojua, sanaa imekuwa mojawapo ya nafasi kubwa za ajira kwa vijana wetu na baaadhi ya wasanii wetu pia wamepata nafasi ya kuperusha bendera ya nchi katika nchi za kigeni, kwa hiyo kusaidia kuitangaza nchi yetu. Tuna imani kuwa kupitia ushirikiano huu tutaweza kuwakutanisha wasanii wetu na mashabiki wao, kuwajengea uwezo na hivyo kuwasaidia wasanii wengi zaidi kufikia viwango vya kimataifa,” anasema Mpinga.

Kwa msimu uliopita, kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ilitoa msaada wa madawati zaidi ya 5,700 kwa maeneo yote ambayo tamasha la Fiesta lilifanyika, madawati hayo yaliweza kufanikisha adhma ya serikali ya kumuinua mtoto toka kukaa sakafuni hadi dawatini.

“Kwa mwaka huu nguvu nyingi tunazielekeza katika kuhakikisha kwamba mtandao wetu unakuwa na nguvu zaidi za kuweza kuzikabili changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikitokea katika maeneo mengi nchini, hii itatuwezesha sisi kuwa mtandao bora na pendwa kwa Watanzania bila kujali maeneo waliyopo,” aliongeza Mpinga.

NANDY

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.