Kobe kuiua jezi namba 24 Lakers

Bingwa - - HABARI/MAKALA -

UONGOZI wa timu ya mpira wa kikapu ya Ligi Kuu Marekani (NBA), LA Lakers, umesema jezi namba 24 haitavaliwa tena, ikiwa ni heshima kwa staa wake, Kobe Bryant, aliyestaafu.

Bryant, mwenye umri wa miaka 39, alistaafu mwanzoni mwa mwaka jana, baada ya miaka yake 20 akiwa na Lakers.

Mpaka sasa Kobe, aliyeanza kuichezea Lakers mwaka 1996, ndiye mchezaji aliyeipatia pointi nyingi Lakers na anashika nafasi ya tatu kwenye orodha ya wafungaji wa NBA, akiwa ametupia mara 33,643.

Kwa mujibu wa timu yake hivyo, jezi hiyo itaachwa rasmi Desemba 18 mwaka huu, siku ambayo itakuwa nyumbani kuvaana na Golden State Warriors.

Bryant anaingia kwenye orodha ya mastaa 10 wa NBA waliostaafu kwa heshima ya jezi zao kutotumika tena. Wengine ni Wilt Chamberlain, Elgin Baylor, Gail Goodrich, Magic Johnson, Kareem Abdul-Jabbar, Shaquille O'Neal, James Worthy, Jerry West na Jamaal Wilkes.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.