Nadal ampotezea Federer

Bingwa - - HABARI/MAKALA -

STAA Rafael Nadal amesema hajawahi kufikiria kuzipiku rekodi za mkali mwenzake katika mchezo wa tenisi, Roger Federer.

Kauli ya Nadal imekuja baada ya kuubeba ubingwa wa US Open kwa kumchapa Kyle Anderson kwa seti 6-3 6-3 6-4 katika mchezo wa fainali.

Nadal sasa amefikisha mataji 16 ya grand slam, huku mpinzani wake huyo wa miaka mingi akiwa na 19.

"Kwa kweli sijawahi kufikiria kuhusu hilo. Nafanya yangu na yeye anafanya yake. Ngoja tuone tutakakoishia,” alisema Nadal. Taji la hivi karibuni la US Open lilikuwa la tatu kwa Nadal, baada ya yale aliyochukua mwaka 2010 na 2013.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.