POCHETTINO AMPA TANO KANE

Bingwa - - SPORTS EXTRA -

KOCHA wa Tottenham, Mauricio Pochettino, amempa tano staa wake, Harry Kane, akisema ni mmoja kati ya mastraika bora duniani, baada ya kinara huyo kufunga mabao mawili katika mchezo ambao waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Borussia Dortmund.

Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Kundi H uliopigwa kwenye Uwanja wa Wembley, Kane alionesha makali kwa kupachika mabao hayo ambayo yalionekana kumkuna vyema kocha huyo. "Kane ni hatari," alisema kocha huyo kupitia mtandao wa UEFA. "Umeweza kuona siku ya leo, kwa kufunga mabao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa ni lazima astahili pongezi,” aliongeza kocha huyo. Alisema kwa upande wake binafsi anamwona kama mshambuliaji bora duniani kutokana na kwamba michuano hiyo ni moja kati ya mikubwa duniani na kitendo cha kufunga bao kinampa sifa anayostahili.

Umeweza kuona siku ya leo, kwa kufunga mabao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa ni lazima astahili pongezi,” aliongeza kocha huyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.