Manusura ajali ya ndege Chapecoense arejea uwanjani

Bingwa - - SPORTS EXTRA -

NYOTA aliyenusurika kwenye ajali ya ndege, Alan Ruschel, amefanikiwa kucheza mechi yake ya kwanza ya mashindano tangu tukio hilo litokee Novemba mwaka jana.

Staa huyo alirejea uwanjani juzi wakati wa mchezo ambao Chapecoense ilitoka sare na Flamengo katika mechi ya kwanza ya michuano ya Kombe la Copa Sudamericana hatua ya 16 bora.

Katika ajali hiyo nyota huyo ni mmoja kati ya wachezaji watatu walionusurika ambapo wengine ni Neto na Jackson Follman, baada ya ndege hiyo iliyokuwa imebeba kikosi kizima cha Chapecoense, benchi la ufundi na baadhi ya waandishi wa habari kuanguka katika eneo la Medellin wakati timu hiyo ikisafiri kwa ajili ya mechi yao ya kwanza ya fainali za Kombe la Sudamericana dhidi ya Atletico Nacional na kusababisha pia vifo vya watu 71.

Kabla ya mechi hiyo, beki huyo mwenye umri wa miaka 28, alirejea uwanjani wakati wa Kombe la Joan Gamper dhidi ya vinara wa La Liga, Barcelona iliyopigwa Agosti mwaka huu katika Uwanja wa Camp Nou na kisha akafanikiwa kufunga bao wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya AS Roma iliyopigwa Septemba mosi mwaka huu.

Hata hivyo, Ruschel alirejea katika mechi za mashindano na kuisaidia Chapecoense kutoshana nguvu dhidi ya Flamengo, mtanange ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Arena Conda.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.