Nagelsmann akana kunyemelea kibarua cha Ancelotti

Bingwa - - SPORTS EXTRA -

KOCHA Julian Nagelsmann, amekana kuwa ananyemelea kibarua cha mwenzake wa Bayern Munich, Carlo Ancelotti, kutokana na kauli alizozitoa hivi karibuni.

Hatua hiyo imekuja baada ya kocha huyo wa timu ya Hoffenheim kuzua tetezi zikidaia kuwa huenda akamrithi Ancelotti kwenye klabu hiyo ya Allianz Arena, baada ya kuuambia mtandao wa Eurosport kwamba familia yake imehamia katika mji wa Munich na kwamba ndio muhimu kwake.

Hata hivyo, akizungumza juzi kabla ya mechi ya Hoffenheim dhidi ya Braga katika michuano ya Ligi ya Europa, kocha huyo alisema hana mpango wa kufukuzia kibarua hicho cha Ancelotti.

"Mada hii imezua mjadala mkubwa tofauti na nilivyotarajia," alisema Nagelsmann. "Kwa bahati mbaya mahojiano yamezua mawimbi ambayo yamemgusa rafiki yangu Carlo Ancelotti ambaye huwa na namheshimu,” aliongeza kocha huyo.

"Ana idadi kubwa ya mataji kwenye kabati lake kuliko niliyonayo. Ila sijawahi kumtumia jumbe Carlo kumwelezea nilikuwa na maana gani kwa kile nilichozungumza,” alikwenda mbali zaidi kocha huyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.