Ukitaka kushuhudia ‘live’ fainali za Kombe la Dunia bei ya tiketi hii hapa

Bingwa - - SPORTS EXTRA -

SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA), limeweka hadharani viingilio vitakavyotumika kununua tiketi katika michezo ya Kombe la Dunia itakayopigwa nchini Urusi mwakani.

Viingilio hivyo vimepanda gharama tofauti na ilivyokuwa kwenye Kombe la Dunia ambazo zilifanyika nchini Brazil mwaka 2014.

Hata hivyo, viwango hivyo vinaonekana kulalamikiwa na wadau wengi wakidai ni vikubwa ikizingatiwa uchumi wa dunia umeporomoka.

Gharama ya tiketi hizo imegawanywa katika makundi saba ambayo ni mechi ya ufunguzi na kila shabiki atalazimika kulipa dola 550, mechi za hatua ya makundi dola 210 na mzunguko wa 16 bora ambapo kila shabiki atajikamua kitita cha dola 245.

Viingilio vingine vilivyotajwa na Fifa ni vya hatua ya robo fainali ambavyo vitakuwa ni dola 365, nusu fainali dola 750 mshindi wa tatu dola 365 na huku kiingilio cha kushuhudia mechi ya fainali kikiwa ni dola 1100.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.