NDIO ZETU

Ronaldo achekelea ushindi Ligi ya Mabingwa

Bingwa - - SPORTS EXTRA -

KWA lugha nyingine unaweza kusema ni kama anachekelea ushindi baada ya straika, Cristiano Ronaldo, kusema michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ndiyo saizi yao, baada ya usiku wa kuamkia jana kuanza vyema kutetea taji lao katika michuano hiyo.

Ligi ya Mabingwa Ulaya ndiyo saizi yao, baada ya usiku wa kuamkia jana kuanza vyema kutetea taji lao katika michuano hiyo.

KWA lugha nyingine unaweza kusema ni kama anachekelea ushindi baada ya straika, Cristiano Ronaldo, kusema michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ndiyo saizi yao, baada ya usiku wa kuamkia jana kuanza vyema kutetea taji lao katika michuano hiyo.

Katika mchezo huo g mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d'Or, alifanikiwa kufunga mabao mawili ambayo yaliwafanya wenyeji hao kuondoka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya APOEL wakiwa katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu.

Akiwa bado anatumikia adhabu ya kutocheza michezo mitano ya ndani kwa kitendo cha kumsukuma mwamuzi wakati wa mechi ya fainali ya Kombe la Supercopa de Espana, Ronaldo alirejea uwanjani akiwa fiti na kufanikiwa kupachika mabao hayo ambayo yamemfanya afikishe 107 katika michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwa sasa Ronaldo na Real Madrid wameelekeza jitihada zao katika michuano hiyo ili kuhakikisha wanalitwaa kwa mara ya tatu taji hilo.

“Bado kuna safari ndefu, lakini ngoja tuianze kwa mechi hadi mechi. Kwanza tuna hatua ya makundi na baada ya hapo tutaona,” Ronaldo alisema kupitia mtandao wa UEFA.com.

“Tupo katika harakati za kutwaa tena ubingwa wa mashindano haya. Mashindano ya Ligi ya Mabingwa ndiyo ya Real Madrid na tunataka kushinda tena,” aliongeza staa huyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.