Pogba kusota benchi wiki sita

Bingwa - - SPORTS EXTRA -

TIMU ya Manchester United, imethibitisha kuwa kiungo wao, Paul Pogba, atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita, baada ya kuumia kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Basel.

TIMU ya Manchester United, imethibitisha kuwa kiungo wao, Paul Pogba, atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki sita, baada ya kuumia kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Basel uliopigwa mapema wiki hii kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, alipatwa na tatizo la nyama za paja katika dakika ya 19 ya mchezo huo kabla ya klabu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Manchester United wamedai kwamba, mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja kabla ya wiki mbili zinazofuata kuanza mazoezi mepesi na anaweza kurudi kwa mara ya kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England dhidi ya Liverpool, Oktoba 14.

Kipindi hiki ambacho mchezaji huyo atakuwa nje ya uwanja, ataikosa baadhi ya michezo kama vile Everton mwishoni mwa wiki hii, Southampton, Crystal Palace pamoja na Kombe la Ligi mzunguko wa tatu dhidi ya Burton na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya CSKA Moscow, Septemba 27.

Hata hivyo, mchezaji huyo atakosa kuitumikia timu yake ya Taifa ya Ufaransa kwenye michezo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi dhidi ya Bulgaria na Belarus mapema Oktoba.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.