Aliyepatia mkeka wa mil. 3 aambulia elfu kumi tu!

Bingwa - - MBELE -

Kwanza mwanakwetu huyu akapiga ile ya uso kwa uso ambayo ilikuwa ni nyekundu kwa nyekundu.

Bila mashaka tena kwa pozi akaisunda nyekundu yake kibindoni kisha akaendelea kupiga kimya wakati huo ndiki zote alizobeti siku hii zimekwisha.

Mwana alikuwa anasikilizia ya Chelsii na Mansiti tu apige milioni zake tatu, kwani aliipa ushindi Mansiti tena wa bao moja hivyo mkeka ulikuwa umetoboa, hapo nazungumzia wikendi ileeee nyingine mwanakwetu si iliyopita.

Mwanakwetu Goodruck Olotu akaanza kuagiza soda za kulevya kwa mbwembwe akiitegemea nyekundu yake kibindoni, huku uhakika zaidi ukiwa ni kwenye mkeka wa mdosi.

Kama kawaida mswazi mwenzangu pombe yake choo baada ya jamaa kuzidiwa kibofuni na wingi ule wa kinywaji ikabidi ainuke kwenda msalani.

Mara akatikisa meza ambayo alikuwa ameweka vilevi ndipo glasi ilipoanguka juu ya mkeka ambao punde alikuwa akiwanywesha wenzake ukawa chapachapa umelowa, alipotaka kuuchukua akajikuta ana vipande vipande vilivyolowa.

Ndipo siku ilipoonekana kuwa ngumu kwa mwanakwetu huyu ambaye badala ya msalani alionekana kuondoka kabisa eneo lile huku akijilaumu, tena hata ndiki yenyewe ilikuwa haijamalizika.

Ikawa hivyo badala ya milioni tatu jamaa akaambulia kumi alafu ile aliyobeti uso kwa uso ambayo pia alitegemea kuilipia vinywaji alivyokuwa anakunywa, turudi mchezoni.

Kama nakuona vile mswazi mwenzangu mate yanavyokutoka ila sijasema uige huu mchezo kwani ni hatari sana. Kama una familia kuna siku unaweza kuwalaza njaa watoto pindi mchezo huu utakapoiteka akili yako ingawa wakati mwingine waswazi wanaifanya ndiyo kazi badala ya zile kamari za karata. Kibaha ni Pwani na Etihad ni chimbo maarufu

kinoma, kipande hiki kwa wanywaji waswazi wa kucheki ndiki, lakini ni maarufu pia kwa wanakwetu wa kudeku muvi za majuu.

Akinyuti kiuchanjaji mlangoni anasimama Hassan Mohamed, lakini Medy Msaka ndiye anayelimiliki chimbo hili, hivyo Hassan anasimama chini yake kama inchaji.

Hili chimbo ndani yake wanazama waswazi 70 pekee lakini siku kinapochafuka waswazi hubebana na kubanana sana kiasi cha kuzama hadi waswazi 100.

Ingawa inakuwa ni hatari kwa afya maana pande hizi kunaonekana hakuna anayejali suala hilo, kwani pamoja na nyomi lililokuwepo wikendi ile kuna waswazi walikuwa wanakula fegi kama kawa yaani bila kujali kama wengine na ule moshi ni tofauti.

Ndani ya Etihad ukija na buku ndiyo mahali pake ingawa kwa mujibu wa inchaji siku kikichafuka cha maana bei huongezeka na kufikia buku jero.

Wana wa huku hawana noma walivyosongoka na ndiki wanakata tu wakati bongo waswazi ukiwapandishia bei kutokana na ukali wa ndiki ugomvi huo oooh!

Tofauti na sehemu nyingi Hassan anasema pande hizi za Kibaha na hasa ndani ya Etihad Stadium, waswazi wanaifuatilia zaidi ligi ya nyumbani.

Inasemekana hata muda aliofika mzee wa Kibandaumiza sehemu hiyo aliwakuta waswazi wengi kwa kuwa walikuwa wakiicheki ndiki ya nyumbani muda si mrefu, hivyo wengi wakaamua kucheki na ile ya majuu na ilichagizwa na ukubwa wake pia.

Unaambiwa ndiki pekee iliyopata kujaza nyomi ndani ya Kibandaumiza cha Etihad msimu huu ni ile ya Yanga na Simba ngao ya jamii.

Ambapo inchaji anakiri licha ya watu wa mtelezo na wazamiaji matembo, lakini kibindoni alikuwa na hela ya maana kuliko siku zote alizoonyesha ndiki Kibandani hapo kwa msimu huu.

Na wewe si una sehemu ya kuonyesha ndiki basi husika na namba hizo hapo juu popote linaposomwa Bingwa, mzee wa Kibandaumiza atakufikia.

Ndipo siku ilipoonekana kuwa ngumu kwa mwanakwetu huyu ambaye badala ya msalani alionekana kuondoka kabisa eneo lile huku..

Mswazi Yohana Zou ambaye alidai ni shabiki lia lia wa Kibandaumiza akijipiga Selfie na mzee wa Kibandaumiza cha Etihad Kilichopo Kibaha mkoani Pwani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.