Banda: Ngoma alikuwa akinipa presha

Bingwa - - HABARI /TANGAZO - NA EZEKIEL TENDWA

BEKI wa zamani wa Simba, Abdi Banda ambaye kwa sasa anaichezea Baroka FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini, amesema straika wa Yanga, Donald Ngoma, alikuwa akimpa presha kubwa kuliko mchezaji mwingine yeyote.

Akizungumza juzi kwenye ofisi za gazeti hili zilizopo Sinza Kijiweni kabla ya kukwea pipa kuelekea Afrika Kusini, Banda alisema alikuwa akiwaza mara mbilimbili namna ya kukabiliana na Ngoma, timu za Simba na Yanga zilipokuwa zikikutana.

“Niseme tu ukweli katika Ligi ya Tanzania nilikuwa na presha ninapoambiwa nakwenda kumkaba Ngoma, kwani ni mchezaji ambaye ana kila kitu lakini nilikuwa napambana hivyo hivyo na mwisho wa siku naweza kumdhibiti.

“Kwa sasa kiwango chake kinaonekana kupungua, nadhani ni kutokana na majeraha yaliyokuwa yakimkabili lakini alikuwa akitupa sana wakati mgumu sisi mabeki wa timu pinzani, nadhani Yanga hawakukosea kumsajili,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.