George Weah anukia urais Liberia

Bingwa - - MBELE -

NA ZAITUNI KIBWANA

IKIWA zimesalia saa chache kabla ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Kagera na Mabingwa watetezi wa Ligi hiyo, Yanga kuchezwa, ‘Wanankurukumbi’ hao ni kama wanataka kufufukia kwenye mchezo huo utakaochezwa katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, baada ya kutamba kuwa hawahofii majina makubwa ya wapinzani wao.

Yanga imepanga kukwea pipa leo asubuhi na kushusha kikosi kizima Bukoba, hali iliyowafanya Kagera kutoa kauli hiyo ya kujihami kwa mabingwa hao.

Kagera imeanza vibaya katika Ligi, ikiburuza mkia baada ya kujikusanyia pointi mbili pekee kwenye michezo mitano iliyoshuka dimbani, hali iliyowafanya viongozi wa timu hiyo iliyomaliza nafasi ya tatu msimu uliopita kukaa kikao na benchi la ufundi kutaka kujua kinaga ubaga.

Wakati Kagera ikiwa inaburuza mkia, Yanga wao wapo nafasi ya sita, wakiwa wameshinda mechi mbili, droo tatu, wakikusanya pointi 9 mpaka sasa.

Beki wa Kagera, Mohammed Fakhi, ambaye msimu uliomalizika jina lake liliteka vyombo vya habari baada ya kudaiwa kucheza akiwa na kadi tatu za njano, aliliambia BINGWA kuwa, kamwe hawahofii majina hayo, hata wakibeba na majeruhi wao wote kuwatisha.

“Tunawasikia mara Amis Tambwe, Obrey Chirwa, ukigeuka huku utasikia Papy Kabamba Tshishimbi, kiufupi sisi hatuogopi majina, hata aje nani tutawaonyesha uwezo wetu, sababu mpira hauangalii majina,” alisema.

Alisema kuwa, kikubwa ambacho wanakifanya kwa sasa ni kuendelea na mazeozi kama kawaida, kuhakikisha wanafanya vema kwenye mchezo huo ili kuondoka na pointi tatu.

“Sisi tunajiandaa na kujipanga, inshallah tutafanya vizuri na tutatoka na pointi tatu, hao wanaotamba na majina na waje, sisi tunaamini kwenye matokeo,” alisema.

Wakati Fakhi akiyasema hayo, Kocha wake, Mecky Mexime, alisema kuwa, mchezo huo ndiyo sehemu ya kupata alama tatu muhimu kufuatia kuanza Ligi kwa kusuasua.

“Sisi hatugawi misaada ya pointi, kama hawajafanya vizuri mechi zilizopita au wana hasira sana na ushindi, hapa si mahala pake, wasitarajie mteremko,” alisema Mexime.

Mchezo huo unategemewa kuwa wa kukata na shoka, kwakuwa timu zote zinahitaji pointi, kwani wakati Kagera ikihaha kujinasua mkiani, Yanga nayo inajipapatua kuhama kwenye nafasi ya sita ambayo haijaizoea.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.