YANGA USHINDI LAZIMA

Yatanguliza makombora Bukoba, kikosi kutua leo

Bingwa - - MBELE -

NA HUSSEIN OMAR

WAKATI kikosi cha Yanga kikitarajiwa kukwea pipa na kuondoka jijini Dar es Salaam leo alfajiri kuelekea Bukoba, tayari viongozi na makomandoo wa klabu hiyo wametua mjini humo ili kuhakikisha piga ua wanaondoka na pointi tatu dhidi ya Kagera Sugar.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, kesho watavaana na wenyeji wao hao kwenye Uwanja wa Kaitaba, ili kusaka ushindi wao wa tatu msimu huu. Msafara wa wachezaji Msafara wa wachezaji 27 wakiwa na Kocha George Lwandamina, ulitarajiwa kuondoka jana, lakini badala yake watapanda ndege leo alfajiri na kutua Bukoba asubuhi, wakitarajiwa kupokewa na viongozi hao na makomandoo.

Vigogo hao na makomandoo wa Yanga walitua Bukoba tangu juzi ili kuhakikisha wanaweka masuala ya ulinzi wa kutosha katika hoteli ambayo wachezaji wao watafika na kuhakikisha hakuna hujuma.

“Tunataka kutetea taji letu la Ligi Kuu, hivyo tumekuja hapa Bukoba tangu juzi Jumatano tukiwa kamili gado. Suala la ushindi ni muhimu kwa kuwa tumejipanga ndani na nje ya uwanja kuwakabili Kagera. Tulisafiri kwa basi la timu na leo asubuhi tunaisubiri timu,” alisema mmoja wa makomandoo wa klabu hiyo.

Akizungumza na BINGWA jana, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, alisema wachezaji wote wa kikosi hicho wataondoka alfajiri (leo) na kwenda Bukoba.

“Tutaondoka na msafara wa watu 27, kila kitu kipo sawa, ila kiungo Thaban Kamusoko na Donald Ngoma tutawaacha kwa kuwa majeruhi. Maandalizi yote yamefanyika na tuna imani kubwa ya kufanya vizuri na kutoka Uwanja wa Kaitaba na pointi tatu,” alisema Hafidh.

Yanga, ambao wamejikusanyia pointi tisa baada ya kucheza michezo mitano, wakishinda miwili na kutoka sare moja na kushika nafasi ya sita, watakutana na upinzani mgumu kwa Kagera Sugar, ambao wanataka kujinasua mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na pointi mbili, baada ya kutoka sare michezo miwili, wakifungwa mitatu kati ya mitano.

Hivyo Kagera wameonekana kupania kuibukia kwa Yanga baada ya hivi karibuni kumweka kitimoto kocha wao, Mecky Maxime, kujadili mwenendo mbovu wa timu hiyo.

Baada ya mchezo huo wa Kagera Sugar, Yanga wataelekea Shinyanga kwa mchezo mwingine dhidi ya Stand United, utakaochezwa Oktoba 22, mwaka huu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.