Savio yatamba kuichapa Pazi

Bingwa - - STORI ZA KITAA -

NA SHARIFA MMASI

IKIWA imebaki siku moja kuunguruma kwa mashindano ya ‘StarTimes Super Cup’, timu ya wanaume, Savio imeapa kuwafunga wapinzani wao, Pazi, watakapokutana kesho alasiri, kwenye uwanja wa Gymkhana, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana, Msemaji wa Savio, Abdul Mtambo, alisema kuwa kikosi chake kimejipanga kushinda michezo yote ili waibuke mabingwa wa mwaka.

“Baada ya kutoa dozi kwenye Ligi ya Kikapu ya Mkoa wa Dar es Salaam (RBA), sasa kazi inahamia kwenye mashindano ya Super Cup yatakayoanza rasmi kesho.

“Kuelekea mashindano hayo, wachezaji wote wapo katika hali nzuri ya ushindani tayari kwa vita kali dhidi ya timu pinzani,” alisema.

Mashindano hayo yanayoshirikisha jumla ya timu sita zilizoshika nafasi za juu kwenye Ligi ya RBA iliyomalizika hivi karibuni, Savio wapo kundi A na timu ya Pazi na Tanzania Prisons.

Wakati kundi hilo mambo yakiwa hivyo, kundi B kuna timu ya Oilers, JKT na Vijana, ambapo bingwa wa mwaka ataibuka na kitita cha Sh milioni mbili.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.