Kocha JKT atoa sababu kufanya vema Nyerere Cup

Bingwa - - STORI ZA KITAA -

NA GLORY MLAY

KOCHA wa timu ya mpira wa wavu ya JKT, Papa Hamisi, amesema sababu ya kuanza vema katika mchezo wao wa kwanza wa michuano ya Kombe la Nyerere dhidi ya Mjimwema, imetokana na wachezaji wenyewe kuwa na umakini mkubwa.

Timu hiyo juzi imeshinda baada ya kuifunga Mjimwema seti 3-2, katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili, hivyo kuwafanya mashabiki kushindwa kutabiri timu gani itashinda, lakini muda ulipomalizika JKT iliitupa nje Mjimwema kwa kuichapa seti hizo.

Katika seti ya kwanza, JKT walipoteza kwa kufungwa seti 25-15, lakini walirekebisha makosa wakashinda seti ya pili kwa pointi 25-19, seti ya tatu pointi 25-21, huku seti ya nne ikichukuliwa na Mjimwema kwa pointi 25-22 na seti ya tano ya ushindi wakachukua JKT kwa pointi 15-10.

Akizungumza na BINGWA jana, Hamisi alisema anapambana kuhakikisha watachukua ubingwa wa mashindano haya kwa mwaka huu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.