Eminem amlipua tena Trump

Bingwa - - TOP TEN TAKWIMU -

LOS ANGELES, Marekani

KIMENUKA! Ndivyo unavyoweza kuanza kusimulia ugomvi mkubwa aliouanzisha rapa Eminem dhidi ya Rais Donald Trump.

Lakini pia, staa huyo wa hip hop hakuishia hapo, amewachana hata mashabiki wake wanaomuunga mkono mwanasiasa huyo.

Iko hivi, Eminem amekosoa maamuzi ya kisiasa ya Trump kupitia mashairi yaliyo kwenye kipande chake cha video chenye urefu wa dakika nne.

Hii si mara ya kwanza kwa Eminem kumkosoa ‘prezidaa’ huyo kwani hata wakati wa hafla ya utoaji tuzo za BET alifanya hivyo.

Katika wimbo huo, rapa huyo anasikika akisema: "Ubaguzi wa rangi ndicho kitu pekee anachofurahia.”

Pia, mbali na kukosoa maisha ya kifahari ya kiongozi huyo, Eminem alipuuzia sera zake, ikiwamo ile ya kupunguza kodi. “Amesema anataka kushusha kodi lakini je, ni nani atakayelipa safari zake za gharama na majengo yake?” alisema msanii huyo.

Alipowageukia mashabiki wake, aliwataka kuamua moja, kama wanamtaka yeye au Rais huyo. “Shabiki wangu yeyote ambaye anamuunga mkono, naweka mstari, kama unamtaka au unanitaka.

"Na kama huwezi kuamua nani unayempenda, nitakusaidia," alisema mkali huyo ambaye mara nyingi amekuwa akiunga mkono vuguvugu za kupinga ubaguzi wa rangi.

Agosti mwaka huu, Eminem aliachia ngoma yake iitwayo FDT, ambayo kwa kiasi kikubwa ilionekana kumpiga vijembe Trump.

Kupitia wimbo huo, mwanamuziki huyo mzaliwa wa Jimbo la California, alisema Trump ni kansa, hivyo hawezi kupewa nafasi ya kufanya maamuzi ya nchi na Wamarekani hawatakiwi kuwa watumwa kwake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.