Serena apania kutetea taji la Australian Open

Bingwa - - TOP TEN TAKWIMU -

FLORIDA, Marekani

MKALI wa tenisi, mwanamama Serena Williams, amedhamiria kuhakikisha analitetea taji lake la michuano ya Australian Open mwakani, taarifa kwa mujibu wa mkurugenzi wa mashindano hayo, Craig Tiley.

Williams, ambaye alifanikiwa kutwaa grand slam yake ya 23 akiwa mjamzito kwenye mashindano ya mwaka huu mapema Januari, alijifungua mtoto wa kike Septemba mosi na kumpa jina la Alexis Olympia Ohanian Jr.

Nyota huyo mwenye heshima kubwa katika mchezo wa tenisi duniani, anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu ya kujiweka fiti ili kutimiza lengo lake hilo.

“Serena atarudi na amepania kutetea taji lake. Hivi ninavyozungumza tayari ameanza mazoezi,” alisema Tiley.

“Jukumu alilonalo kwa sasa ni kuhakikisha anajiweka fiti zaidi ndani ya hii miezi michache kabla ya mashindano kuanza.”

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.