BATA TU! ‘AMSHA DUDE’

Bingwa - - IJUMAA - NA KYALAA SEHEYE

HABARI zenu washkaji zangu wa kona yetu hii ya Hapa Bata Tu, najua mtakuwa mko poa na mnaendelea vizuri na michakato mbalimbali ya maisha hasa siku kama ya leo ambayo mnakamilisha majukumu yenu kwa ajili ya kuanza wikiendi.

Kama kawaida ya Hapa Bata Tu, siku ya leo tunakuorodheshea maeneo mbalimbali ambayo utakwenda kupumzika wikiendi hii baada ya uchovu wa kazi nzito ambazo umefanya wiki nzima.

Katika maeneo hayo utakwenda kupumzisha akili na kutuliza mawazo na kuliamsha dude kwa kula bata za kutosha na marafiki zako au familia yako.

UWANJA WA CCM KIRUMBA MWANZA Kesho katika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kutakuwa na ‘show’ bab kubwa ya Muziki Mnene, ambapo wasanii kama Snura Mushi, Madee, Young Killer, TID na wengine wengi wa Singeli Fleva watakuwapo.

MBEYA CITY PUB Baada ya Tamasha la Tigo Fiesta ‘Tumekusoma’ kupita mikoa mbalimbali kama Mwanza na Arusha, leo itakuwa zamu ya Jiji la Mbeya, ambako wakazi wa ‘Green City’ watajiachia ndani ya City Pub kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwamo mkongwe wa muziki wa hip hop na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.

GARDEN BREEZMAGOMENI HOSPITALI

Kama kawaida ‘Family Bonanza’ litaendelea katika viwanja hivi vya Garden Breez kila Jumapili, ambapo Khalid Chokoraa atakuwa na bendi yake ya Mapacha Watatu.

EQUETAR GRILL- MTONI KWA AZIZI ALLY Bendi ya Zanzibar Stars Modern Taarab watakuwa wakitoa burudani katika ukumbi huu kila Jumapili, ambapo watashirikiana na waimbaji chipukizi wa Mtoni Music.

MLIMANI CITY - CENTURY CINEMA Filamu ya The Emoji bado itaendelea kuonyeshwa leo katika ukumbi huo, pia filamu zilizofanya vizuri Agosti zitaonyeshwa pia.

RIVER ROADKIBAHA PICHA YA NDEGE Leo kutakuwa na ‘live band’ katika ukumbi huo ambapo watapiga nyimbo yoyote ambayo shabiki ataomba kupigiwa. Kesho kutaporomoshwa disko bab kubwa kutoka kwa Madj wakali wa ‘club’ ya ukumbi huo.

BONAG HOTEL- KILUVIA GOGONI

Leo kutakuwa na shindano la kucheza sebene na vijana 20 watapanda jukwaani kuonyeshana uwezo wao, mshindi atalamba shilingi 200,000 na zawadi nyingine zitatolewa kwa mshindi wa pili hadi wa nne.

Kesho itakuwa ni zamu ya muziki wa dansi utakaopigwa na bendi ya ukumbi huo. MAONI NA USHAURI TUMA SMS

KWA 0712-616155

Filamu ya The Emoji bado itaendelea kuonyeshwa leo katika ukumbi huo, pia filamu zilizofanya vizuri Agosti zitaonyeshwa pia.

Snura Mushi

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.