Cyju Bwax apata menejimenti

Bingwa - - IJUMAA - NA MWANDISHI WETU

MSANII wa Bongo Fleva, Cyju Bwax (Mzee wa Kitonga), amesema ana furaha kubwa kupata menejimenti itakayokuwa inasimamia kazi zake za muziki ikiwa ni muda mrefu umepita toka alivyofanya kazi zake mwenyewe. Akizungumza na Papaso la Burudani, Cyju Bwax, alisema uongozi wake mpya unaoitwa Perfect Sound ambao unamiliki studuio kubwa na ya kisasa maeneo ya Ubungo, Dar es Salaam ambapo atakuwa na uhakika wa kuufikisha mbali muziki wake. “Baada ya kugundua mtaani kuna vipaji vingi ikiwemo kuimba ndipo walipoamua kufanya kazi na mimi, kwa kuanza tutaachia wimbo wangu wa kwanza unaoitwa Naishi Stoo ambapo video yake itafanywa na mwongozaji Eddy, bila shaka itakuwa rahisi kwangu kutusua,” alisema Cyju.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.