Ben Pol aingiza sokoni albamu yake

Bingwa - - IJUMAA - NA MWANDISHI WETU

STAA wa muziki wa RnB nchini, Benard Paul ‘Ben Pol’, juzi aliingiza sokoni albamu yake ya tatu inayokwenda kwa jina la ‘The Best of Ben Pol’ yenye mjumuiko wa nyimbo zake zote zilizowahi kufanya vizuri.

Ben Pol ameliambia Papaso la Burudani kuwa umefika wakati wa wasanii kuacha woga wa kutotoa albamu kwa sababu zisizo na mashiko zinazofanya tasnia ya muziki isikue na mashabiki wasipate burudani wanayostahili.

“Nimetoa albamu yangu mpya nikiwa naamini Tanzania bado kuna wanunuaji, ndani yake kuwa nyimbo zangu zilizowahi kufanya vizuri na nyingine mpya kabisa kwa hiyo mashabiki wanaweza kuipata kwenye mitandao yote inayouza nyimbo,” alisema Ben Pol.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.