MURRAY, DJOKOVIC KUNOGESHA AUSTRALIAN OPEN

Bingwa - - HABARI - CANBERRA, Australia

VINARA wa tenisi kwa upande wa wanaume na wanawake, Andy Murray na Novak Djokovic watashiriki michuano ya Australian Open ambayo itafanyika Januari mwakani.

Mkurugenzi Mkuu wa michuano hiyo, Craig Tiley, alisema jana kwamba nyota hao watashiriki michuano hiyo, baada ya kuwa nje ya uwanja kutokana na sababu mbalimbali.

Alizitaja sababu hizo kuwa Mwingereza anayeshika nafasi ya kwanza kwa ubora, Murray, hajaingia uwanjani tangu Julai mwaka huu, baada ya kutenguka kiganja katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Wimbledon wakati Djokovic alikuwa na matatizo ya goti.

Tiley alisema nyota hao wawili wataungana na Novak Djokovic na Stan Wawrinka.

"Wachezaji wote nyota watakuwapo kwenye michuano hiyo ya Melbourne," alisema mkurugenzi huyo.

Wawrinka na Nishikori, nao walikuwa hawajacheza tangu majira ya joto yaliyopita kwa kile kinachosemekana ni matatizo ya goti na kiungio cha kiganja na mkono.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.