LeBron shakani kuanza mechi za ufunguzi NBA

Bingwa - - HABARI - NEW YORK, Marekani

STAA wa mpira wa kikapu, LeBron James, ataikosa mechi ya mwisho ya Cleveland Cavaliers kujiandaa na msimu ujao na kuna wasiwasi huenda akaikosa mechi ya ufunguzi wa Ligi ya NBA dhidi ya Boston Celtics kutokana na majeraha ya enka yanayomkabili.

Straika huyo aliteguka enka wakiwa mazoezini kabla ya mchezo waliofungwa vikapu 108-94 dhidi ya Chicago Bulls ambao ulipigwa mwanzoni mwa wiki hii.

Staa huyo sasa anaonekana ataikosa mechi ya leo ambayo watakutana na Orlando Magic.

"Kwa leo hakuweza kufanya mazoezi. Kwa uzoefu wangu na kesho (jana) hatafanya hivyo kutokana na Ijumaa sitamchezesha nasikitika sana lakini sina jinsi,” alisema kocha mkuu wa timu hiyo, Tyronn Lue.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.