Kubica aruka kiunzi cha kwanza

Bingwa - - HABARI - LONDON, England

DEREVA mahiri wa zamani wa mbio za magari aina ya langalanga, Robert Kubica, ni kama ameruka kiunzi cha kwanza kati ya viwili, baada ya juzi kukamilisha jaribio la kwanza katika timu ya Williams ambayo inamfanyia majaribio ili kuona kama anaweza kurejea katika mbio hizo za Formula 1.

Staa huyo hajawahi kushiriki mchezo huo tangu mwaka 2011 alipopata ajali mbaya ambayo ilimuacha na jeraha kubwa kwenye bega lake la kulia.

Hata hivyo, jana timu hiyo ya Williams ilieleza kuwa staa huyo wa zamani wa timu za BMW Sauber na Renault, anaonekana atafanya vizuri baada ya kushiriki mbio hizo za Silverstone akiwa na gari ya mwaka 2014.

Mtihani wa pili kwa Kubica mwenye umri wa miaka 32, unatarajiwa kuwa katika mbio za Hungaroring, lakini timu hiyo ya Williams haikutaja zitafanyika lini.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.