‘Bishoo’ Adriano kurejea uwanjani

Bingwa - - IJUMAA -

KILA mmoja anatamani kumdhibiti mp enzi wake. Kila mmoja anataka mpenzi wake asimuwaze mtu mwingine ila yeye tu. Anataka yeye ndiye awe mtawala wa akili na hisia za mwenzake.

Akianza kuhisi mpenzi wake, kwa namna yoyote ile anamwona mtu mwingine hasa wa jinsia tofauti naye, ni bora sana ni wa maana kuliko yeye, anapoteza furaha, anakuwa na huzuni na kutawaliwa na msongo wa mawazo.

Ili mtu afurahie mapenzi ni lazima ahisi mwenzake anamwona yeye ni kila kitu katika maisha yake. Bila kuwa na hisia hizi, hakuna mtu anayeweza kujidai sana kuwa na mwenzake.

Mapenzi ni hali ya kuhisi na kuamini una thamani sana katika maisha ya mtu. Yaani uhisi anakuona wewe ni mtu maalumu sana, wa maana sana na wa thamani sana kuliko wengine.

Si vibaya kuwaza hivi. Mapenzi ndiyo yako hivi. Shida ipo katika njia za kufanya mtu azidi kukuwazia katika mrengo huu. Ifahamike kuwa, kama uko na mtu mwenye kukupenda na kukujali kwa dhati, kitu cha msingi unachotakiwa kukifanya ili aendelee kukuthamini na kukujali kwa kiwango unachotamani ni kucheza na akili yake na si kuwa mbabe kwake ama kumbana sana.

Hapa ndipo tatizo la wengi. Wengi baada ya kuingia katika mapenzi, baada ya kujua wanawapenda sana wenzao, hudhani njia nzuri ya kuwadhibiti ni kuwabana sana na kuwafuatilia kwa karibu mno. Njia hii si sahihi hata kidogo.

Kumbuka mwenzako ni binadamu kama wewe. Mwenzako anahitaji nafasi ya kufurahia uhuru wake na maisha yake kama wewe. Ndio, anahitaji kuwa na mipaka. Inabidi maisha yake yaoneshe utofauti kati ya zamani kabla hajawa na wewe na sasa baada ya kuwa na wewe.

Ila hiyo haiondoi ukweli kuwa mwenzako bado ni binadamu. Binadamu mwenye utashi na maamuzi. Yeyote akibanwa sana uhisi anaonewa na akitawaliwa na hisia hizi kwa muda mrefu ujue hawezi kukuona wewe kama chanzo cha furaha yake.

Unatakiwa kuishi kwa akili na mwenzako na si ubabe. Unatakiwa kutokuwa ‘mnoko’ sana katika baadhi ya mambo. Dharau baadhi ya mambo ya kijinga. Ukiwa unafuatilia kila kitu kwa makini sana, sio tu utamnyima mwenzako fursa ya kufurahia ubinadamu wake ila hata wewe utajinyima fursa ya kufurahia maisha yako.

Wapo baadhi ya watu, wenzao wakichelewa kupokea simu kesi huwa kubwa hata bila kuwapa nafasi ya kujitetea. Ni kweli simu ya mkononi inatakiwa kuwa karibu na mhusika. Ila si kila muda.

Akienda chooni ataenda nayo? Akiwa anafua atakuwa nayo? Akiwa katika mbinyano ndani ya daladala anawezaje kuitoa na kuwasiliana na wewe wakati kusimama kwenyewe kasimama kwa mguu mmoja?

Ukifuatilia kwa karibu sana hata kwa mambo madogo utajikuta unasababisha migogoro na gomvi zisizo na lazima kila siku katika uhusiano wako. Kama binadamu inabidi ujue mwenzako ana mapungufu na uzembe wake. Vitu hivi ndivyo vinavyokamilisha ubinadamu wake.

Mwenzako angekuwa kamili kwa kila kitu asingeitwa binadamu. Angeishi mbinguni huko na malaika wenzake na wewe usingemwona. Acha kumbana sana, acha kuumia kwa mambo madogo.

Watu wanahitaji kufurahi katika uhusiano wao na si kuzongwa zongwa ama kukosewa kila muda. Alivyokubali kuwa na wewe alijua anakuwa na mpenzi mwenye kumjali na kumthamini. Si kuwa na mwalimu au nyapara wa kufuatilia kila kitendo chake kwa karibu na kukikosoa ovyo.

Ijulikane hakuna mtu ambaye huwa na utulivu akiwa na mtu mwenye kupenda sana kumkosoa, kumsema sema ama kumzodoa. Watu wanapenda kuwa karibu na watu wenye kuona ubora na thamani zao zaidi kuliko wanavyoona makosa yako.

Sasa kwanini unakuwa kero kwa mpenzi wako badala ya kuwa raha na faraja? Unyapara haufai kupelekwa katika mapenzi. Watu wanatafuta raha na amani na si kufanywa kujiona wajinga na wa ovyo.

Ndiyo, kuna mambo ya kurekebishana, ila sasa ndiyo kila muda uongelee mapungufu yake? Kila muda unamsema yeye tu? Wewe uko safi sana? Huna makosa? Huna mapungufu? Mwenye busara huwa anatumia macho yake mawili kwa ufasaha.

Moja huwa linaona mapungufu ya mwenzake na lingine linaona ubora wa mwenzake. Maana yake ni kwamba kuna wakati anamkosoa mwenzake japo huwa kwa lugha sahihi ila pia kuna muda anamsifia mwenzake na kumfanya ajione wa thamani na bora sana katika maisha yake.

Acha kuwa mlalamishi. Acha kumfanya mwenzako ajione kama mnyama wa kufugwa. Mpe nafasi walau, acha kumkosoa kwa kila kitu. Kuna vitu mwenzako anafanya kwa bahati mbaya, vitu hivi hata ukiacha kumkosoa atajirekebisha mwenyewe.

Kukosoana sana kunafanya watu waogopane katika mapenzi. Sasa kama mnaogopana mtafurahia vipi mapenzi? Haiwezekani.

Kuna wakati inabidi umfanye mwenzako awe huru sana na wewe.

Sio akikuona anaanza kupata mchecheto. Ili mapenzi yavutie inabidi kila mmoja amuone mwenzake kama rafiki, mpenzi na mtani. Sasa ukimkosoa sana badala ya kukufikiria katika mtazamo huu, yeye atakuona kama mwalimu ama mzazi wake. Hapa mtafurahia vipi mapenzi yenu?

Mwandishi wa makala hii ni mtaalamu mbobezi wa masuala ya ushauri wa uhusiano, maisha na utulivu wa hisia (Psychoanalyst).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.