BEKI ANAWA MIKONO KWA LUKAKU, KANE

Uwanja wa Shah Alam ambao upo katika mji wa Shah Alam nchini Malaysia, ni kati ya viwanja vikubwa 20 duniani ukiwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 80,372. Uwanja huu ulizinduliwa mwaka 1994 na ndio unaotumiwa na timu ya Ligi Kuu nchini humo, Super League,

Bingwa - - MBELE - LIMA, Peru

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Colombia, Radamel Falcao, amekiri madai ya kuwashawishi wachezaji wa Peru wasifunge bao na kuyaacha matokeo yabaki 1-1 kwenye mechi yao ya mwisho ya kufuzu Kombe la Dunia mapema wiki hii.

Falcao alitupiwa lawama kwa kitendo chake cha kuzungumza na wachezaji wa Peru na kuwaambia wasitumie nguvu kufunga bao la pili na sare hiyo ikaipeleka Colombia moja kwa moja Urusi huku Peru ikilazimika kucheza mechi za mchujo dhidi ya New Zealand.

“Tulikuwa tunafahamu kilichokuwa kinaendelea kwenye mechi nyingine, tulicheza na matokeo hayo na ndio maana nilijaribu kuwashawishi na wachezaji wa Peru,” alisema Falcao mara baada ya mchezo huo.

Falcao alionekana kumnong’oneza kitu nyota wa Peru, Renato Tapia, ambaye naye alikiri wazi lakini alikanusha kuwa ni kitu kilichoandaliwa.

“Katika dakika tano za mwisho, Wakolombia walitufuata. Walituambia hali halisi iliyokuwa ikiendelea kwenye mechi nyingine, Falcao aliniambia kuwa sote tulishafuzu (kama msimamo ulivyo), lakini ndio soka,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.