Wenger kumpoza machungu Sanchez

Bingwa - - SPORTS EXTRA - LONDON, England

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema kuwa haamini kama huzuni ya Chile kukosa tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia mwakani itaathiri kiwango cha mshambuliaji wake, Alexis Sanchez.

Sanchez alisikitishwa na matokeo ya kubamizwa mabao 3-0 na Brazil kwenye mechi ya mwisho ya kufuzu, huku matokeo ya mechi nyingine nayo yakichangia kwa kiasi kikubwa kwa Chile kutoenda Urusi mwakani. “Itabidi nizungumze naye,” alisema Wenger alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari kuelekea mechi yao na Watford wikiendi hii.

“Jana (juzi) niliitazama mechi yote na ninalazimika kusema anatakiwa kupatiwa uangalizi zaidi. Mechi ilikuwa ngumu kimwili na kiakili, nitasimamia hilo suala.”

Wenger aliongeza: “Sanchez ni kama Aaron Ramsey, ni washindani hasa. Akili zao zinafikiria kushinda tu. Lakini kwa sasa hawatacheza Kombe la Dunia hivyo wanatakiwa kuirudisha akili yao kwenye klabu.”

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.