Vertonghen anawa mikono kwa Lukaku, Kane

Bingwa - - SPORTS EXTRA - LONDON, England

KITASA wa klabu ya Tottenham, Jan Vertonghen, amefunguka wazi kuwa anajisikia fahari kucheza kwenye timu zilizo na mastraika Romelu Lukaku na Harry Kane, akiamini wapachika mabao hao watakuwa na vita kali ya kuwania kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu msimu huu.

Vertonghen aliiongoza Ubelgiji mapema wiki hii dhidi ya Cyprus, ambapo Lukaku alifunga moja ya mabao manne na kufikisha mabao 16 ndani ya mechi 13 msimu huu.

Beki huyo amerejea kwenye kikosi cha Spurs na kuungana na Kane, ambaye alifunga mabao mawili katika mechi za timu yake ya taifa.

Kane amepachika mabao 15 katika mechi 10 za mwisho na Vertonghen alikiri kuwa anajiona mwenye bahati kukutana na washambuliaji hao hatari kwenye mazoezi tu, ingawa Lukaku yuko Man United na siku si nyingi timu hizo zitakutana.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.