MKE WA BRAVO AWAVAA MASTAA CHILE

Bingwa - - SPORTS EXTRA - SANTIAGO, Chile

BAADA ya kushuhudia matumaini ya Chile kushiriki michuano ya Kombe la Dunia mwakani yakififia, mke wa nahodha na mlinda mlango wa timu hiyo, Claudio Bravo, amewashukia mastaa wa kikosi hicho kwa kulewa kizembe na kushindwa kucheza vizuri.

Chile ilishindwa kukata tiketi ya michuano hiyo kufuatia kichapo cha mabao 3-0 walichokipata dhidi ya Brazil kwenye mchezo wa mwisho, sambamba na matokeo ya Argentina kuifunga Ecuador, matokeo yaliyomkasirisha kimwana Carla Pardo na kuwashukia mastaa hao kwa kuposti Instagram.

“Niishukuru timu ya taifa kwa nyakati zote maalumu. Nimshukuru nahodha wangu (Bravo) kwa yote uliyotufanyia.

“Pale jezi inapovaliwa lazima kuwe na heshima na ndio maana kuna waliojifua vilivyo kabla ya mechi na wengine wakaenda kula bata na kushindwa kufanya mazoezi kwa sababu ya ulevi, lakini kwa sasa tuungane kwenye machungu kama taifa.”

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.