MATA AWATOLEA NJE WACHINA

Bingwa - - SPORTS EXTRA - inatoka 24

Weah, mwenye umri wa miaka 51 kwa sasa, tayari ana cheo cha useneta katika nchi yake hiyo ya Liberia na yu mbioni kuwa rais wa nchi hiyo.

Ni asilimia zaidi ya 50 ya kura zinazotakiwa kwa mgombea mmoja kushinda urais nchini Liberia, na imetajwa kuwa ndiyo sababu ya matokeo hayo kucheleweshwa.

Kiasi kikubwa cha watu walimpigia chapuo Weah kuingia Ikulu kati ya wagombea 20 wanaowania kuchukua kiti cha mwanamama, Ellen Johnson Sirleaf.

Weah aliitumikia Chelsea katika mechi 15 na kufunga mabao matano, akiichezea kwa mkopo kutoka Milan mapema mwaka 2000. Alijiunga na City mwaka huo huo lakini alicheza mechi tisa tu baada ya kuzozana na kocha, Joe Royle.

Straika huyo aliwahi kutwaa mataji lukuki akiwa na Milan, PSG na Monaco, pia akilitumikia taifa lake la Liberia katika mechi 60.

Sam Mannah, mjumbe wa timu ya kampeni ya Weah, alisema: “Weah yupo katika hali nzuri sana na ana hamu ya uongozi. Kila mtu anamwambia kwamba mabadiliko ni lazima.

“Mwaka 2005 aligombea, ila walisema hana uzoefu, lakini kwa sababu ana cheo cha useneta, wamemkubali.

“Maisha yake ya zamani ya soka yamemsaidia sana. Waliberia wanakumbuka mengi mazuri kutoka kwake. Zamani alilisaidia taifa, akaziwezesha hospitali, alitoa misaada ya chakula na kuwasaidia watu kwenda Marekani na hata kuwalipa wachezaji wa timu ya taifa.

“Watu wanafahamu yote aliyowahi kuyafanya, wanamuona mwenye uwezo wa kubadilisha maisha yao.”

Aidha, mmoja wa wahariri wa gazeti la Liberia, Othello Garblah aliandika: “Weah ni maarufu sana. Aliahidi kupiga vita rushwa na kuendeleza elimu sambamba na kubuni fursa za kazi.

“Wagombea wote wana mipango hiyo hiyo, hivyo wapiga kura watachagua kulingana na haiba. Umaarufu wa Weah umetokana na maisha yake ya soka.”

Kwa mujibu wa mtandao wa The Sun, uchaguzi huo unafanyika kwa mizunguko kadhaa na matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutoka wikiendi hii.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.