Mchana nyavu Lipuli aikazia uzi Yanga SC

Bingwa - - TANGAZO - NA ZAINAB IDDY

MSHAMBULIAJI wa Lipuli, Ditram Nchimbi, amepata tetesi za kuendelea kuhitajika na Yanga lakini amesema atakuwa tayari kujiunga katika klabu hiyo kwa masharti aliyowapa.

Yanga wanajipanga kukiboresha kikosi chao ili kiweze kutetea taji la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, ambapo kwa sasa wanawania saini ya mshambuliaji huyo.

Akizungumza na BINGWA jana, Nchimbi alisema atakuwa tayari kusaini Yanga, iwapo watatimiza masharti aliyowapa ya kuhakikisha anapata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha kocha George Lwandamina.

Nchimbi alisema kwa sasa ana mkataba wa mwaka mmoja na Lipuli na Yanga wakimhitaji watatakiwa kukaa meza moja na viongozi wa klabu hiyo ili kuona namna ya kuuvunja.

“Nilichohitaji kwa Yanga katika usajili wa dirisha kubwa ni wao kukubali nipate nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza na si kukaa benchi,” alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.