TAIFA STARS ITUPE FARAJA

Bingwa - - MAONI MTAZAMO KATUNI -

TIMU ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kesho inatarajia kucheza na wenyeji Benin katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotambuliwa kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kwa wanachama wake kucheza na taifa jingine.

Mechi hiyo tunaona ni muhimu kwa Taifa Stars kushinda, kwa kuwa itasaidia Tanzania kupanda katika viwango vya soka vya ubora vinavyotolewa na Fifa kwa kila mwezi.

Kwa maana hii, wachezaji wa Taifa Stars wafahamu kwamba mchezo huo ni muhimu kupata matokeo mazuri ambayo yataipaisha Tanzania katika viwango vya soka duniani na kutoka nafasi inayoshika sasa ya 136.

Tunaamini kwamba kucheza na timu ya Taifa ya Benin ambayo iko nafasi ya 79 katika viwango vya Fifa na kushinda, itatoa nafasi kubwa kwa Tanzania kupanda nyingi katika viwango vya soka duniani.

Tunacheza na Benin baada ya mwezi uliopita kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Malawi katika mchezo wa kirafiki pia wa kimataifa uliokuwa kwenye kalenda ya Fifa uliochezwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, hivyo hatutarajii Taifa Stars ikifungwa au kupata sare na wenyeji kesho pamoja na kwamba watakuwa ugenini wakicheza mbele ya mashabiki wa wapinzani wao.

BINGWA tunaamini kwamba, kikosi kilichoitwa na kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga, kina uwezo mkubwa wa kupata matokeo mazuri wakiwa ugenini, lakini kitu kikubwa wanachotakiwa ni kupambana kuhakikisha wanawapa faraja Watanzania.

Ni imani yetu kwamba, Taifa Stars imeandaliwa vizuri na kilichobaki kwa Watanzania ni kuona wanapata wanachokitarajia kutoka kwa wachezaji wa timu hiyo.

Tunaamini kabisa, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Serikali na wadau na Watanzania kwa ujumla kila mmoja yuko nyuma ya Taifa Stars kuhakikisha inarejea nchini na ushindi.

Tunamaliza kwa kusema kwamba, Taifa Stars wanatakiwa kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu na kujituma katika dakika zote 90 ili wenyeji Benin wasipate nafasi ya kufunga. Tunaitakia kila la heri Taifa

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.