Ruvu kusajili wanne Bara, Zanzibar

Bingwa - - HABARI/MATANGAZO -

NA TIMA SIKILO

KLABU ya soka ya Ruvu Shooting, inatarajia kufanya usajili wa wachezaji wanne katika usajili wa dirisha dogo litakalofunguliwa rasmi kesho kutwa ili kuimarisha kikosi chao.

Wachezaji watakaosajiliwa watatoka katika klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara na visiwani Zanzibar ili kuiongezea nguvu timu yao.

Akizungumza na BINGWA jana kocha wa timu hiyo, Abdulmutic Hadj, alisema kikosi chake kina mapungufu katika maeneo matatu, hivyo anahitaji kusajili wachezaji wanne ambao wataziba pengo la beki wa kati, washambuliaji wawili na winga mmoja.

“Tumefanya tathmini na kuona timu yetu ina mapungufu, hivyo tunahitaji kufanya usajili kulingana na mahitaji yetu muhimu ili kukiongezea nguvu kikosi na kujiridhisha tupo vizuri katika kufanikisha malengo yetu.

Kocha huyo alisisitiza kuwa hawatasajili wachezaji wanaocheza ligi za madaraja ya chini kwani wanahitaji wale wa Ligi Kuu, lakini kwa sasa hawezi kuweka wazi majina yao wala timu wanazotoka.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.