TUNA IMANI NA KAMATI YA MAANDALIZI AFCON U-17

Bingwa - - MTAZAMO MAONI KATUNI -

SERIKALI imeunda kamati ya watu 25, ambayo itaanza kufanya maandalizi ya fainali za Afrika (Afcon), kwa vijana walio chini ya miaka 17 zitakazofanyika mwaka 2019 hapa nchini.

Kamati hiyo ilitangazwa jijini Dar es Salaam juzi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, inayotakiwa kuanza kufanya kazi mara moja kwa kuwa mwaka 2019 si mbali.

Kutokana na umuhimu wa michuano hiyo, kamati hiyo itakuwa chini ya uenyekiti wa Mwakyembe mwenyewe huku Henry Tandau, ambaye ni Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), kuwa Mtendaji Mkuu.

Wengine ni rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodger Tenga, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Makamu wa Rais wa TFF, Michael Wambura, Mwanasheria Damas Ndumbaro, Dk. Francis Michael na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Khamis Kigwangalla.

Katika kamati hiyo pia wamo Aboubakar Bakhresa, Yusuph Omary, Ahmed Mgoyi, Khalid Dallah, Nasib Mbaga, Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Angetile Osiah na Dk. Alan Kijazi,

Dk. James Dotto ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Kamishna wa Uhamiaji, Dk. Ana Peter, Fred Manoki, Lameck Nyambaya, William Erio, Kelvin Twisa, Mohamed Dewji, Ladislaus Matindi na Devota Mdachi.

Kwanza, tunampongeza Waziri Mwakyembe kwa kuunda kamati ambayo sisi BINGWA tunaamini itafanya kazi nzuri kwa kuwa inaundwa na watu makini, wenye weledi mkubwa, lakini uzoefu wao ni mkubwa katika sekta ya michezo na nyingine.

Hatuna shaka kabisa na uteuzi uliofanywa na Waziri Mwakyembe kwa wajumbe wa kamati hiyo, kwa kuwa tunafahamu uzoefu wa kazi kwa baadhi ya wajumbe waliomo kwenye kamati.

BINGWA tunaamini kwamba, kamati ya maandalizi ya fainali hizo haitamwangusha Waziri Mwakyembe na Watanzania kwa ujumla kwani wanachohitaji ni kuona maandalizi yake yanakamilika kwa asilimia 100.

Ni kweli kama alivyosema Waziri Mwakyembe kuwa Tanzania kuandaa fainali za Afrika kwa vijana ni heshima kubwa kwa Taifa, hivyo kamati ihakikishe inakamilisha kila kitu ndani

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.