Oxford watinga sita bora Temeke

Bingwa - - HABARI -

NA TIMA SIKILO

OXFORD wamefanikiwa kutinga hatua ya sita bora, baada ya kuifunga mabao 3-1 Faru Boys katika mechi ya Ligi Daraja la Tatu Wilaya ya Temeke, uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Mabatini, jijini Dar es Salaam.

Ilikuwa dakika ya 25 kwa Saidi Kinyonya kuipatia Oxford bao la kuongoza kabla ya Faru Boys kusawazisha dakika ya 45 kupitia nahodha wa timu hiyo, Shafii Bilal.

Oxford waliongeza bao la pili dakika ya 66 kupitia kwa Chikaka Chikaka na baadaye Kinyonya tena alifunga bao la tatu kwa shuti kali.

Akizungumza na BINGWA juzi nahodha wa Faru Boys, Bilal alisema mechi hiyo ilikuwa ngumu kwa upande wao, ingawa walitengeneza nafasi nyingi za kufunga.

“Tumekubali matokeo wenzetu walifanikiwa kuzitumia nafasi, tumefungwa tutaangalia tulipokosea na kurekebisha makosa yetu ili tuweze kushinda mechi zitakazofuata,” alisema Bilal.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.