Makatta: Alliance ni timu bora

Bingwa - - HABARI -

NA MASYENENE DAMIAN, MWANZA

MBWANA Makatta ambaye ni kocha wa timu ya Alliance FC, amesema kikosi chake ni bora kutokana na kimesheheni vijana wengi wenye vipaji vya soka.

Alliance inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL), inaongoza katika Kundi C, baada ya kuibuka na ushindi wa bao 4-1 dhidi ya Toto Africans katika mchezo uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza.

Ushindi huo umeiwezesha Alliance kufikisha pointi 19 ikiishusha kileleni Dodoma FC inayobaki na pointi 18, baada ya kupoteza kwa kufungwa 1-0 na Biashara United katika mchezo uliochezwa juzi katika uwanja wao wa nyumbani.

Akizungumza na BINGWA jijini hapa, Makatta alisema kikosi chake ni bora zaidi na kilistahili ushindi mnono wa kuanzia mabao sita mpaka saba dhidi ya Toto Africans.

"Nashukuru mechi imeisha tumeshinda, kuna wakati vijana wangu waliridhika wanawaruhusu wapinzani kurudi mchezoni, lakini hili ni kosa ambalo tutalirekebisha liko zaidi kwenye ‘psychology’, tunatakiwa tuendeleze spidi ya mchezo kwa kushambulia sana ili tupate mabao mengi kwenye uwanja wa nyumbani.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.