Karate wapeana majukumu mazito

Bingwa - - HABARI -

NA ESTHER GEORGE

SHIRIKISHO la Mchezo wa Karate Tanzania (TFK), limeweka mikakati na viongozi kupeana majukumu mazito ili kuhakikisha mchezo huo unapiga hatua kitaifa na kimataifa. Akizungumza na BINGWA jana, Mwenyekiti wa TFK, Sensei Willy Ringo, alisema katika kikao chao kilichofanyika juzi, jijini Dar es Salaam, walikubaliana kila mmoja kutekeleza majukumu ili kuleta mafanikio ndani ya chama hicho.

Ringo alisema katika kikao hicho walikubaliana kila kiongozi kutekeleza wajibu na majukumu yake, kwani ushirikiano utaleta nguvu.

“Tumekubaliana kuwa mkakati wetu uliotukusanya ni kujenga upya mchezo huu ili usonge mbele na kuleta manufaa katika nchi yetu hivyo ni wajibu wa kila kiongozi kutekeleza jukumu lake kwa muda mwafaka,” alisema.

Katika hatua nyingine, alisema klabu zinatakiwa kuwaandaa wachezaji wao kabla ya mashindano ili kupata kikosi bora.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.