Unaambiwa Bale ameumia mara 24 akiwa Madrid

Bingwa - - KOLAMU -

MADRID, Hispania

WINGA wa klabu ya Real Madrid, Gareth Bale, ameripotiwa kuwa jeraha alilopata mwishoni mwa wiki iliyopita lilikuwa ni la 24 tangu ahamie hapo Juni 2013.

Bale ni mmoja wa wachezaji ambao kuumia mara kwa mara kwao limekuwa kama jambo la kawaida na majeraha hayo mara nyingi ni misuli tena bila kuguswa na mtu.

Hata hivyo, jeraha kubwa zaidi bila shaka ni la enka ambalo lilimlazimu winga huyo kufanyiwa upasuaji na kushindwa kucheza mechi 17, karibu msimu mzima uliopita, ikiwa ni rekodi mbaya zaidi tangu aanze kucheza soka.

Katika kuongezea hilo, Bale alikosa mechi nyingine 10 kutokana na matatizo ya misuli.

Msimu wa 2015/16, Bale alikosekana kwenye mechi 19, zote kwa sababu ya maumivu ya msuli; msimu wa 2013/14, alikosa tena mechi 15. Msimu huu tayari ameshakosa mechi tisa na jumla.

Kwa mujibu wa mtandao wa takwimu wa Opta, Madrid imemkosa Bale kwenye mechi 91 kati ya 250 za michuano yote tangu walipomsajili kutoka Tottenham, hiyo ikiwa ni asilimia 36.4 ya mechi zote hizo.

Maeneo ya mwili wake ambayo yamekuwa yakiumia kila mara ni ‘Soleus’ (moja ya misuli ya kigimbi) na paja lake la kushoto.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.