Majambazi wateka timu ya Mercedes

Bingwa - - KOLAMU -

RIO, Brazil

DEREVA wa mbio za magari aina ya langalanga maarufu kama Formula 1 Lewis Hamilton, amewataarifu viongozi wa timu ya Mercedes kwamba kikosi chao kilishambuliwa kwa risasi kabla ya kuanza mashindano ya Brazilian Grand Prix.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 32 ambaye alitwaa ubingwa wa dunia wiki iliyopita nchini Mexico, alisema jana kwamba tukio hilo lilitokea Ijumaa wiki iliyopita wakati wakitoka katika Uwanja wa Sao Paulo wakirejea hotelini kwao.

Hata hivyo, alisema hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa, lakini baadhi ya vitu vyao muhimu viliibiwa ndani ya basi ya timu yao kabla ya kufanyika mbio hizo zilizoanza jana.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.