Zimefuzu ila zitaibeba Afrika Kombe la Dunia 2018 ?

Bingwa - - JUMATATU SPESHO -

NA JESCA LUTEGO (TSJ)

WAKAZI wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake, usiku wa kuamkia jana Jumapili, walipata burudani ya aina yake waliposhuhudia Tamasha la Tigo Fiesta likifanyika kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, huku wasanii 14 waliopanda jukwaani wakifanya shoo ‘bab kubwa’.

Katika tamasha hilo ambalo limefunga hesabu ya Tigo Fiesta kwa mikoani mwaka huu, alikuwa ni msanii Genevieve Mpangala ambaye ni Miss Tanzania 2010, aliyefungua pazia kwa kufanya shoo ya aina yake kabla ya wakali wanaounda kundi la Rostam, yaani Roma na Stamina kufunga shoo hiyo.

Ama kwa hakika lilikuwa ni tamasha la aina yake kutokana na jinsi wasanii walivyofanya kile kilichokuwa kikitegemewa na mashabiki na hivyo kukonga vilivyo nyoyo zao kuwafanya kutojutia muda na fedha zao.

Kama ilivyo kawaida yake katika matamasha ya mwaka huu, msanii Aslay ndiye aliyekuwa kinara mjini Mtwara kwa kuwapagawisha mashabiki waliojaa kwa wingi uwanjani hapo.

Mbali ya Aslay, Rostam na Genevieve, wasanii wengine waliopanda jukwaani mjini humo usiku wa kuamkia jana ni Chege, Maua Sama, Jux, Madee, Jux, Lulu Diva, Snura, Janjaro na wengineo.

Akizungumzia tamasha hilo, Meneja wa Mauzo Tigo Kanda ya Kusini, Uthman Madatta, alisema: “Tunashukuru msimu huu Tigo Fiesta kutufikia mkoani Mtwara na watu wamejitokeza kwa wingi sana, lakini pia ndani ya msimu huu tumeweza kuwafikia wananchi wa maeneo ya Masasi, Newala na Tandahimba kuwezesha kuuza korosho zao kwa kupitia huduma ya Tigopesa bila ya kupata usumbufu wa kusafiri umbali mrefu kwenda kwenye mabenki.

“Hii inaonyesha jinsi gani tunajali wateja wetu waondokane na usumbufu popote walipo kwa kuwa tumejikita zaidi kidijitali.”

Tamasha lijalo la Tigo Fiesta ambalo ndilo funga pazia msimu huu, linatarajiwa kufanyika Jumamosi ya Novemba 25, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Lulu Diva Aslay Genevieve Mpangala Madee Janjaro

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.