Chiellini Msomi wa Chuo Kikuu anayewatesa washambuliaji Serie A

Bingwa - - JUMATATU SPESHO -

MILAN, Italia

UKIWATAJA mabeki wanaong’ara Ligi Kuu nchini Italia ‘Serie A’, bila shaka utamgusia pia Giorgio Chiellini wa Juventus ambaye licha ya umri wake, bado ameendelea kuwa tegemeo kwenye safu ya ulinzi ya timu hiyo.

Chiellini beki wa kati ambaye ni mzaliwa wa Livorno, amejizolea umaarufu mkubwa Serie A kutokana na ukabaji wake unaowafanya washambuliaji wa timu pinzani kushindwa kufurukuta.

Muitalia huyo ameichezea Juve katika mechi 341, akifunga mabao 25 tangu alipojiunga na timu hiyo mwaka 2005 akitokea Fiorentina aliyoichezea mwaka mmoja.

Kwa ufupi, historia ya mlinzi huyo katika soka inaanzia katika msimu wa 2000–2002 alipojiunga na Livorno ambayo hata hivyo aliichezea mechi nane pekee kwa kipindi chote cha miaka miwili alichokaa klabuni hapo. Baadaye, Roma aliporudishwa Livorno kwa mkopo.

Safari yake ya ustaa

Akiwa katika klabu yake hiyo ya zamani, aliweza kung’ara, akicheza mechi 47 na kufunga mabao manne. Hapo, Fiorentina wakavutiwa na huduma yake na kufanikiwa kumchukua kwa mkopo.

Akiwa Fiorentina, aliweza kufanya vizuri kwani alicheza mechi 37 na hapo ndipo Juve walipomnasa mwaka 2005.

Hata hivyo, nje ya soka baba huyo wa mtoto mmoja wa kike aitwaye Nina, ni msomi wa Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara (Master’s in Business Administration).

Chiellini aliipata elimu hiyo mwaka huu baada ya kuwa na Shahada ya Usimamizi ya Biashara aliyoipata mwaka 2010 katika Chuo Kikuu cha Turin.

Kutokana na elimu yake hiyo, wengi wametabiri kuwa huenda akapewa shavu la kusimamia masuala ya biashara katika klabu yake ya Juve endapo ataamaliza maisha yake ya soka.

Alianza soka akiwa kiungo

Mashabiki wengi wanamfahamu kwa ustadi wake anapocheza kama beki wa kati, lakini hiyo si nafasi aliyoanzia safari yake ya soka. Wakati anajiunga na klabu yake ya utotoni ya Livorno, kipindi ambacho alikuwa na umri wa miaka sita, Chiellini alikuwa kiungo mshambuliaji. Baadaye, alionekana pia kuzimudu nafasi za beki wa kushoto na winga.

Kumng’oa Juve bil 65

Nyota huyo anayetumia zaidi mguu wa kushoto, amekuwa akitajwa kutakiwa katika klabu za Chelsea na Manchester City kila dirisha la usajili linapofunguliwa.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mitandao inayojihusisha na tafiti za uchambuzi wa thamani ya wachezaji kwenye soko la usajili, Chiellini anagharimu euro milioni 25, takribani Sh bil 65 za Tanzania.

Udhaifu wake Licha ya kwamba Chiellini ni mmoja kati ya mabeki bora barani Ulaya, bado ana mapungufu yake uwanjani, kwa mujibu wa wachambuzi wa soka barani humo.

Tatizo kubwa la beki huyo ni tabia yake ya kupenda kushambulia, ni mwepesi mno kusogea kwenye eneo la ulinzi la timu pinzani. Wachambuzi wanaamini kuwa hiyo inaweza kuigharimu safu ya ulinzi ya timu yake, hasa pale anapokuwa amekwenda mbele.

Kisa kung’atwa begani na Suarez

Tukio hilo lilitokea kwenye mchezo wa Kundi D katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014, ambapo ni Italia ilikuwa inacheza na Uruguay ya staa Luis Suarez.

Ulikuwa ni mtanange kwa pande zote mbili na matokeo yake yangeamua timu ambayo ingevuka na kutinga hatua ya 16 bora na ni Uruguay ndiyo iliyoibuka na ushindi wa bao 1-0.

Katika dakika ya 79, Suarez alionekana akiwa kwenye ulinzi mkali wa Chiellini wakati wakiwa kwenye eneo la hatari la Italia wakisubiri mpira wa krosi na ndipo straika huyo alipoonekana akimng’ata mwenzake.

walimnasa lakini kwa miaka mitatu aliyokaa kwenye timu hiyo, hakucheza hata mchezo mmoja na ndipo

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.