MESSI kuikosa Nigeria kesho

Bingwa - - JUMATATU SPESHO -

BUENOS AIRES, Argentina

MASHABIKI wa timu ya Taifa ya Argentina hawatamuona nyota wao, Lionel Messi, akiwa uwanjani katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Nigeria ‘Super Eagle’ utakaochezwa kesho nchini Uturuki.

Nahodha huyo alicheza kwa dakika zote 90 katika mtanange wa juzi dhidi ya wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia za mwakani, Urusi, ambapo Argentina walichomoza na ushindi wa bao 1-0 mjini Moscow.

Hata hivyo, hatakuwa uwanjani kuisaidia timu yake hiyo itakapomenyana na Super Eagles, mchezo wa maandalizi ya michuano hiyo itakayoanza kutimua vumbi wakati wa majira ya kiangazi ya mwakani.

Taarifa za Messi mwenye umri wa miaka 30 kutosafiri na kikosi cha kocha Jorge Sampaoli na badala yake kurejea kwenye klabu yake ya Barcelona, imetolewa na Chama cha Soka cha Argetina (AFA) kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter.

Lakini, taarifa hiyo haikuweka wazi kilichomzuia Messi kuwavaa Wanigeria, ikifahamika wazi kuwa mchezaji huyo si majeruhi.

Itakumbukwa kuwa hayo yanakuwa mapumziko ya kwanza kwa Messi, kwani amecheza kila dakika tangu kuanza kwa msimu huu wa La Liga.

Baada ya mchezo wao dhidi ya Urusi, mfungaji bora huyo wa Argentina alimpongeza staa mwenzake katika kikosi cha Argentina, Sergio Aguero ambaye licha ya hivi karibuni kuweka rekodi ya kuwa mpachikaji mabao wa muda wote wa Man City, juzi aliingia ‘top three’ ya wafungaji wa muda wote Argentina.

Taarifa za Messi mwenye umri wa miaka 30 kutosafiri na kikosi cha kocha Jorge Sampaoli na badala yake kurejea kwenye klabu yake ya Barcelonam..

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.