MASTAA

VIGOGO EPL WALIVYOKICHAFUA MECHI ZA KIMATAIFA

Bingwa - - HABARI -

LONDON, England

KIVUMBI cha Ligi Kuu England (EPL) kilipumzishwa kwa muda ili kupisha mechi za kimataifa za kirafiki na zile za kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwakani nchini Urusi.

Hata hivyo, bado ilikuwa ni burudani kwa mashabiki wa EPL kwani walihamishia macho kwa mastaa wa ligi hiyo waliokuwa na mataifa yao. Je, ni mastaa gani waliozibeba timu zao za Taifa kwa kipindi hiki cha mapumziko ya ligi mbalimbali barani Ulaya?

Giroud (Arsenal)

Straika huyo aliifungia Ufaransa katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wales, mchezo uliochezwa jijini Paris. Katika kikosi hicho cha Ufaransa kulikuwa pia na beki Laurent, huku Alexandre Lacazette akitokea benchi.

Pia, kinda Eddie Nketiah, aliifungia timu ya U-19 ya England ilipoichapa Iceland mabao 2-1 katika mchezo wa kuwania kwenda Euro ya makinda wenye umri huo.

Lakini pia, Granit Xhaka, aliyekuwa na Uswisi, aliiongoza timu hiyo kushinda bao 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Ireland, mchezo uliokuwa wa ‘play-offs’ kufukuzia nafasi ya kwenda Urusi mwakani.

Mesut Ozil alicheza kwa dakika zote 90 wakati timu yake ya Taifa ya Ujerumani ikimaliza mchezo kwa kutofungana na England.

Hazard, Morata (Chelsea)

Staa Eden Hazard aliyekuwa na kikosi cha Ubelgiji, alifunga bao la kwanza katika sare ya mabao 3-3 dhidi ya Mexico.

Huku ikiwa hivyo kwa Hazard, Alvaro Morata naye alikuwa na Hispania, ambapo naye alipachika bao katika ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Costa Rica.

William, ambaye alikuwa nahodha wa Brazil, alihusika katika upatikanaji wa bao la tatu alilofunga Gabriel Jesus katika ushindi wao wa mabao 3-1 dhidi ya Japan.

Aguero, Silva (Man City)

‘Babu’ David Silva alifunga mara mbili wakati timu yake ya Hispania ikiitambia Costa Rica kwa ushindi wa mabao 5-0.

Sergio Aguero naye alifunga bao pekee wakati Argentina walipoilaza Urusi bao 1-0.

Kwa upande wake, Danilo aliyekuwa na ‘uzi’ wa Brazil ndiye aliyepiga krosi ya bao la tatu la mwisho lililofungwa na Gabriel Jesus, katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Japan.

Kevin De Bruyne alikuwa na Ubelgiji katika mchezo dhidi ya Mexico, lakini aliitwa benchi baadaye, huku Bernardo Silva akicheza kwa dakika zote za mchezo akiwa na Ureno walioichapa Saudi Arabia mabao 3-0. Lukaku, Romelu mabao mawili mabao 3-3 Mkhitaryan (Man United) Lukaku aliifungia Ubelgiji katika mchezo wao wa sare ya dhidi ya Mexico. Kwa mabao hayo, Lukaku aliweza kuifikia rekodi ya aliyekuwa mfungaji bora wa muda wote kwenye timu hiyo. Henrikh Mkhitaryan, naye alikuwa na Armenia na ndiye aliyeifungia timu yake hiyo bao la pili walipoimaliza Belarus kwa mabao 4-1. Kwa upande mwingine, Victor Lindelof, aliiongoza safu ya ulinzi ya Sweden kutoruhusu bao katika mchezo walioichapa Italia bao 1-0.

Son (Tottenham) Nyota Heung-min Son, alizipasia nyavu mara mbili na kuipa Korea Kusini ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Colombia. Katika mchezo huo wa kirafiki, Son alikuwa anakabiliana na mchezaji mwenzake katika kikosi cha Tottenham, Davinson Sanchez, ambaye alikuwa na ‘uzi’ wa Colombia. Eric Dier alivaa kitambaa cha unahodha wa England kwa mara ya kwanza ingawa hawakufungana na Ujerumani, Kieran Trippier, alianza lakini aliitwa benchi katika dakika ya 72 na nafasi yake kuchukuliwa na Kyle Walker. Mousa Dembele aliingia kipindi cha pili wakati timu yake ya Ubelgiji ikitoka sare ya mabao 3-3 na Mexico. Serge Aurier aliyekuwa na Ivory Coast alishindwa kuiokoa timu yake hiyo kupokea kichapo cha mabao 2-0 na Morocco, hivyo kuikosa nafasi ya kwenda Urusi mwakani.

Staa Eden Hazard aliyekuwa na kikosi cha Ubelgiji, alifunga bao la kwanza katika sare ya mabao 3-3 dhidi ya Mexico.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.