Unajua kwanini Neymar hafurahii maisha PSG?

Bingwa - - HABARI -

PARIS, Ufaransa

HALI si shwari kwa staa Neymar katika klabu yake mpya ya PSG na hilo limethibitika juzi baada ya nyota huyo kumwaga chozi mbele ya waandishi wa habari mjini Rio, Brazil.

Hata uongozi wa Real Madrid umeligundua hilo ndio maana umeanza kumnyemelea kujua endapo ataamua kufungasha kila kilicho chake na kuondoka PSG.

Juzi, akiwa Brazil alikokwenda kujiunga na timu yake ya Taifa, Neymar alilia wakati kocha wake, Tite alipokuwa anazungumzia mustakabali wake pale Paris.

Kwa mujibu wa wachambuzi, kilichomliza Neymar ni ukweli kwamba hafurahii maisha mapya nchini Ufaransa.

Kwanza, amekuwa akikerwa na tetesi za mara kwa mara kutoka kwa vyombo vya habari kuwa haelewani na staa mwenzake kikosini, Edinson Cavani na hili la hivi karibuni kuwa haivi na kocha wa timu hiyo, Unai Emery.

Hata mchezaji huyo amekiri kuwa anaumizwa na tetesi zinazoenea kwani hazina ukweli na kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikimnyima raha. "Kuna stori zinazonivuruga ambazo si za kweli. Sina tatizo na kocha wala Cavani," alisema. Pili, Neymar ameikumbuka familia yake, hasa mtoto wake aitwaye David Lucca ambaye bado anaishi Barcelona na dada na mama yake ambao wanaishi Brazil. Tatu, kuna tatizo la lugha, ambapo inaelezwa kuwa Kifaransa kimekuwa kikimpa wakati mgumu Mbrazil huyo pindi anapotaka kuwasiliana na wenzake. Tayari Madrid wanasikilizia kinachoendelea kati ya Neymar na PSG, huku kukiwa na tetesi kwamba wameshatenga kitita cha euro milioni 200 (zaidi ya Sh bil 500) kuhakikisha wanamnasa hapo mwakani.

Kwanza, amekuwa akikerwa na tetesi za mara kwa mara kutoka kwa vyombo vya habari kuwa haelewani na staa mwenzake kikosini, Edinson Cavani na hili la hivi karibuni kuwa haivi na kocha wa mu hiyo, Unai Emery.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.